INDIA WAJITOA KWENYE KOMBE LA DUNIA NI BAADA YA KUZUIWA KUCHEZA MPIRA WAKIWA PEKU
- Kombe la dunia mwaka huu
ndio kombe la kwanza la dunia kutumia teknolojia ya goli ( goal-line
technology) kwani haijawahi tokea kombe lolote la dunia ambalo limewahi kutumia
teknolojia hii zaidi ya kutumia uwezo binafsi wa marefa na vibendera.
- katika fainali zote mashindano ya kombe la
duniani zilizo wahi kuchezwa ni fainali mbili tuu ambazo ziliamuliwa
kwa mikwaju ya penati fainali hizo ni za mwaka 1994 pale Brazil
walipoifunga Italy na fainali nyingine ni ya mwaka 2006 pale Italy
ilipoifunga France
- Mpaka leo hii kombe la dunia linatimiza miaka 80 huku
likizunguka katika nchi mbalimbali na mabara mbalimbali lakini kombe la kwanza la dunia lilifanyika katika
nchi ya uruguay mwaka 1930 na nchi kumi na tatu (13) zilishiriki
- Vivian Richards raia wa antigua ndiye
mwanamichezo pekee duniani kucheza na kushiriki kombe la dunia akiwa
na timu mbili za michezo tofauti alishiriki kombe la dunia kama mchezaji
wa mpira wa miguu mwaka 1974 katika mechi za kufuzu, pia ni nguli nchini
mwao katika mchezo wa cricket ambako pia ameshawahi kushiriki katika
kombe la dunia la cricket.

- Mashindano ya kombe la dunia ndiyo mashindano
maarufu kuliko yote na yenye watazamaji wengi zaidi duniani kila mwaka
yanapofanyika, mashindano hayo hutazamwa na watu zaidi ya bilioni nne
duniani kote.
- ·
licha ya Ujerumani kuifunga
Brazil goli saba moja katika kombe la dunia mwaka 2014 lakini haishikirii
rekodi ya kufunga magoli mengi katika kombe hilo , timu inayoshika rekodi kwa
kufunga magoli mengi katika mechi moja ni Hungary ambayo iliifunga El
Salvador magoli 10 – 1 mwaka 1982.

- ·
Haya kweli ni maajabu ya kombe la
dunia usishangae watoto wa kibongo wakicheza chandimu wakiwa peku nchi ya
India ilijitoa katika mashindano ya kombe la dunia mwaka 1950 pale uongozi wa
FIFA ulipowazuia kucheza peku katika mechi zao.

No comments:
Post a Comment