Tuesday, August 12, 2014

CHADEMA YAFUKUZA MAKADA MBALIMBALI KWA TUHUMA ZA KUTAKA KUKIGAWA CHAMA,MBUNGE VITI MAALUMU AHUSISHWA............

Katika kikao cha kamati ya jimbo kilichoketi jana kiliibuka na maamuzi mazito na mema kwa uhai wa chama ambapo Maliselina simbasana diwani viti maalum (kagu) amevuliwa uanachama na kamati kuu jimbo la Geita kwa tuhuma za kukihujumu chama hicho akishirikiana na makada kadhaa wa chama hicho ambao walikuwa ni viongozi ndani ya chama hicho.

Hatu hiyo ya kumnyang'anya kadi ya chama imekwenda sambamba na kuwaandikia barua wanachama washirika wa Marcelina ambao ni:

Daudi sunzu katwale mjumbe kutoka mkoa wa geita kwenda ziwa magharibi

Gabriel Nyasilu mwanachama

Focus Mpogomi mwanachama

Deogratus shinyanga mwanachama


Mabula ndoshi mwenyekiti kitongoji cha tambukareli

Jackon j Mabula mwanachama

Mutta Robert mwanachama

Yukuli dandali mwanachama

Happy Bwenge mwanachama

Josephine mwika mwenyekiti wa chama Kata ya mtakuja

Barua inawataka wajieleze kwanini wasifukuzwe uanachama?

Makosa wanayotuhumiwa nayo ni KUKIGAWA cha kwa kushirikia na Mbunge wa CCM Vick Kamata kukihujumu chama hicho, ambapo idara ya ulinzi ya chama iliwasilisha ushahidi wa video na sauti jambo lililopolekea watuhumiwa kukiri kosa.

Kuwatusi viongozi wa kanda mitandaoni tena kwa kutumia Id (Mutta Robert mwanachama) zao halisi, kuwatusi viongozi wa jimbo bila kufikisha malalamuko yao kwenye vikao husika.

Kuiba nyaraka za chama na kuzipeleka kwa Vick Kamata wa ccm.

Kufanya vurugu kila inapotakiwa kuitisha vikao vya kamati kata na wilaya.

Kuunda mtandao wao wakugombea ubunge Geita kinyume na utaratibu, idara ya ulinzi imejiridhisha pasina shaka (kwa vielelezo) kuwa walikuwa wakifadhiriwa na Vick Kamata wa ccm kwa malengo ovu dhidi ya chadema.

No comments:

Post a Comment